Kanisa linatumia vyombo vya habari kama njia ya kuwafikia watu wengi zaidi kwa ujumbe wa Injili na taarifa za maisha ya kanisa.
Kupitia redio, televisheni ya mtandao, mitandao ya kijamii na machapisho, waumini na jamii kwa ujumla wanapata mahubiri, vipindi vya kiroho na habari za matukio ya kanisa.
Kanisa pia linawajengea uwezo vijana katika fani za habari na mawasiliano.
Shughuli Kuu
- Vipindi vya redio
- Televisheni ya mtandao na matangazo mubashara
- Mitandao ya kijamii na tovuti
- Machapisho na majarida ya kanisa