Idara ya Ukaguzi wa Ndani inahakikisha kwamba rasilimali za kanisa zinatumika kwa uaminifu, uwazi na kwa mujibu wa sera na taratibu zilizowekwa.
Idara hufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa hesabu na mifumo ya udhibiti katika ofisi kuu, majimbo na taasisi za kanisa, na kutoa mapendekezo ya kuboresha.
Kazi hii inasaidia kujenga imani ya waumini na washirika kwa uongozi wa kanisa.
Shughuli Kuu
- Ukaguzi wa hesabu na mifumo ya udhibiti
- Ushauri kuhusu usimamizi wa fedha
- Kufuatilia utekelezaji wa mapendekezo
- Mafunzo ya uwajibikaji kwa watumishi