Idara ya Wanawake na Watoto inaratibu huduma za kiroho na kijamii kwa wanawake na watoto katika majimbo yote ya kanisa.
Kupitia mikutano, semina na vikundi vya wanawake, idara inawajenga wanawake kiroho, kiuchumi na kiuongozi. Pia inasimamia huduma ya Shule ya Jumapili na malezi ya watoto.
Idara inashirikiana na wadau mbalimbali katika kupinga ukatili na kulinda haki za watoto.
Shughuli Kuu
- Mikutano na semina za wanawake
- Vikundi vya kiuchumi vya wanawake
- Shule ya Jumapili na malezi ya watoto
- Kulinda haki za watoto