Injili ya Kristo inagusa maisha yote ya mwanadamu. Kwa sababu hiyo, kanisa linatekeleza miradi inayolenga kuboresha hali ya maisha ya jamii inayolizunguka.
Miradi hii inahusisha upatikanaji wa maji safi na salama, kilimo bora na ufugaji, vikundi vya kuweka akiba na kukopa, pamoja na msaada kwa yatima, wajane na wazee.
Jamii inashirikishwa tangu hatua ya kupanga hadi utekelezaji ili kuhakikisha miradi inakuwa endelevu.
Shughuli Kuu
- Miradi ya maji safi na salama
- Kilimo bora na ufugaji
- Vikundi vya kuweka akiba na kukopa
- Msaada kwa yatima, wajane na wazee
- Mafunzo ya ujasiriamali