Moravian Church in Tanzania
About Us

Our History

Safari ya Kanisa la Moravian Tanzania na mizizi yake ya karne nyingi.

The Origin of the Moravian Church in Tanzania

The Origin of the Moravian Church in Tanzania
The Moravian Church was officially founded in 1457 by followers of the religious reform movement associated with the martyr John Hus . It is one of the oldest Protestant denominations in the world, with more than 500 years of history When it was first established, its official name was the “Unity of the Brethren” ( Unitas Fratrum). However, many years later, during the 18th century, it became widely known as the Moravian Church. The name “Moravian” was adopted because many of its early members came from the region of **Moravia**, which is now part of the **Czech Republic**. Throughout its long history, the Moravian Church has played an important role in the global Protestant community. It has also been recognized for its early commitment to making the **Bible available in the languages spoken by ordinary people**, rather than limiting Scripture to classical languages such as Greek and Latin. The Moravian Church has therefore maintained a strong tradition of **faith, education, mission, Bible translation, and service to communities** across the world.
Kanisa hili lilikuwa la kwanza kuchapisha nyimbo za kitabuni kwa lugha za wananchi wenyeji. Pia kanisa hili lilikuwa la kwanza kuweka msisitizo wa kuelimisha wanawake na wanaume; na walikuwa waanzilishi wa vuguvugu la misheni (Uinjilisti) ya Kiprotestanti tangu mwaka 1732. Wamoravian wamekuwa mstari wa mbele katika kukuza Umoja wa Kikristo katika historia yao yote, na ni mmoja wa waanzilishi wa Baraza la Makanisa Ulimwenguni ( WCC), na Umoja wa Kikristo Tanzania (CCT). Kituo cha kwanza cha misheni cha Moravian Tanzania kilianzishwa Rungwe Kusini mwa Tanzania mwaka 1891. Kituo kingine upande wa Magharibi mwa Tanzania kilikabidhiwa kwa Bodi ya Moravian huko Herrnhut, Ujerumani, na Shirika la Wamisionari la London (LMS) mwaka 1897. Ni kutokana na matokeo ya kazi ya uinjilisti ya vituo hivi viwili, kanisa la Moravian lilienea katika maeneo ya kusini na na magharibi mwa Tanzania na nchi nzima, kila moja lilikuwa na jimbo lake.
Haja ya kuanzisha ushirikiano kati ya Jimbo la Kusini na Magharibi ilionekana tangu mwanzo wa kuanzishwa kwao. Wamisionari waanzilishi walikuwa wameanzisha mawasiliano mapema kuanzia 1899. Baadaye walianza kukutana na kubadilishana uzoefu na majimbo hayo mawili na wakaanzisha ushirikiano katika mambo mbalimbali. Mnamo 1965 walikubaliana kuunda rasmi Bodi ya pamoja ili kujadili na kukubaliana juu ya mambo ya msingi kwa majimbo yote mawili. Mnamo 1968 majimbo haya mawili yaliamua kuanzisha kwa pamoja Chuo cha Theolojia cha Moravian ( MOTHECO) kwa ajili ya mafunzo ya wachungaji; na mwaka 2004 kilisajiliwa rasmi kama Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji ( TEKU). Mwaka wa 1976 Jimbo la Kusini liligawanywa mara mbili na hivyo kuwa Jimbo la Kusini na Jimbo la Kusini Magharibi, na hali hiyo hiyo ilifanyika kwa jimbo la Magharibi mwaka 1986 na kuwa Jimbo la Magharibi na Jimbo la Rukwa. Tangu wakati huo, mpaka wakati huu Kanisa la Moravian nchini Tanzania lina majimbo nane (8) na Majimbo ya Misheni mawili (2). Pamoja na kuundwa kwa majimbo hayo mapya haja ya kuanzisha Kanisa la Moravian Tanzania kama chombo cha kitaifa cha kuratibu na kuunganisha kazi hiyo ikawa kubwa zaidi. Chombo hiki kingeweza kusimamia kwa pamoja programu mbalimbali za majimbo na kuwakilisha majimbo ndani na nje ya nchi.
Mnamo tarehe 04 Agosti 1986, wajumbe kutoka majimbo manne ya Tanzania walikutana Sikonge na kuazimia kuanzisha rasmi Kanisa la Moravian Tanzania (KMT) kama chombo cha kuwaunganisha Wamoravian wote nchini Tanzania. Mnamo 23 Novemba 1986, KMT ilizinduliwa rasmi mwezi Aprili 1987 ilisajiliwa rasmi katika mamlaka za serikali ya Jamhuri ya Tanzania. KMT ilitambuliwa rasmi na Sinodi ya Umoja wa Ndugu (Unitas Fratrum) katika mkutano mkuu wake huko Antigua, West Indies mwaka 1988. KMT inawakilisha majimbo mbele ya serikali, makanisa mengine, mashirika mbalimbali, na mashirika ya kiekumene. Zaidi ya yote, jukumu lake kuu ni kupitia majimbo ni kuhubiri Injili Takatifu ya Wokovu ndani na nje ya kanisa. KMT pia inasimamia taasisi zote zinazomilikiwa na majimbo kwa pamoja. Pia linafanya programu mbalimbali za kiroho na za kijamii. Miongoni wa programu hizo ni pamoja na kutoa elimu kupitia taasisi zake, semina na warsha mbalimbali. Kutoa elimu ya theolojia, uuguzi na utabibu, ufamasia, Ufundi, Uinjilisti, pamoja na taaluma mbalimbali ili kuchochea maendeleo katika jamii ya Kitanzania pamoja na nchi jirani. Programu kuu za kanisa ziko katika eneo la mafunzo ya wachungaji na wainjilisti kwa ajili ya uinjilisti na umisionari.
>> Donate

Your generous offerings support the ministry of the Moravian Church, thank you!

Your gift supports worship, evangelism, spiritual leadership, and the church's mission to serve our community. Every offering helps spread the Gospel and meet the needs of others.

Every gift enables the Moravian Church Tanzania to continue our mission of building one family of God through preaching, teaching, and service.

"Each of you should give what you have decided in your heart to give, not reluctantly or under compulsion, for God loves a cheerful giver."

— 2 Corinthians 9:7
Donate >>